Search This Blog

Sunday, May 16, 2021

Tetesi za soka Ulaya leo 16/05/2020

Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amekiambia kikosi chake kuwa ataondoka mwishoni mwa msimu huu.(Goal)


Kocha wa Everton Carlo Ancelotti na meneja wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri ni miongoni mwa wanaofikiria kuchukua nafasi ya Zidane ikiwa ataondoka klabuni humo. (Sunday Mirror)

Manchester City wameambiwa wanaweza kumsajili mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 33, kutoka Barcelona ikiwa watamlipa Pauni 500,000 kwa wiki baada ya kukatwa ushuru (Sun on Sunday)

Manchester United inamtaka kiungo wa Ufaransa Paul Pogba, 28, kutia saini kandarasi mpya lakini wanahofia mshahara ambao wakala wake, Mino Raiola, anajaribu kumpatia mteja wake(Sunday Mirror)

Everton wako tayari kumuuza mlinzi wa Uingereza Mason Holgate, 24, ili kukusanya pesa za kumsajili beki wa kati wa wa senegal Kalidou Koulibaly, 29, kutoka Napoli (Football Insider)

Mshambuliaji wa Lyon na Uholanzi Memphis Depay, 27, yuko mbioni kujiunga na Barcelona.(L'Equipe - in French)

Mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 32, anamezewa mate na Paris St-Germain ikiwa ataamua kuondoka Bayern Munich. (L'Equipe - in French)

Liverpool haitamsaini beki wa kati wa Uturuki Ozan Kabak kwa mkataba wa kudumu msimu huu wa joto. Mchezaji huyo wa miaka 21 alijiunga nao kwa mkopo kutoka Schalke mnamo Februari (Sun on Sunday)

Arsenal wanatarajia kuishinda Manchester City katika kumsajili beki wa kushoto wa England mwenye umri wa miaka 31 Ryan Bertrand, ambaye ataondoka Southampton mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu. (Mail on Sunday)

Newcastle inamfuatilia mshambuliaji wa Leeds na Wales mwenye umri wa miaka 22 Tyler Roberts. (Football Insider)

West Ham wana nafasi nzuri ya kumsaini mlinda lango wa West Brom mwenye umri wa miaka 28 Sam Johnstone, ambaye pia anahusishwa na Tottenham (Football Insider)

Kocha wa Barcelona aliye chini ya shinikizo Ronald Koeman amekutana na rais wa kilabu Joan Laporta na anasema wawili hao watazungumza tena mwishoni mwa msimu (Goal)

Eintracht Frankfurt wanalenga kumteua mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid Raul kuwa meneja wao kwa msimu ujao (Marca)

Villarreal wapo mstari wa mbele kumsajili beki wa pembeni wa Barcelona na Brazil Emerson. Kijana huyo wa miaka 22 yuko kwa mkopo Real Betis (Mundo Deportivo - in Spanish)

Real Madrid wana nia ya kumsajili kiungo wa Ufaransa Eduardo Camavinga kutoka Rennes, na Arsenal pia inamtaka mchezaji huyo wa miaka 18(Marca)

Bayern Munich na Borussia Dortmund wanamfuatilia mshambuliaji wa Sheffield United mzaliwa wa Canada aliye katika kikosi cha england cha wachezaji wa chini ya miaka 18, Daniel Jebbison, 17 (90 Min)

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...