Search This Blog

Wednesday, May 12, 2021

Tetesi za Soka Ulaya leo 13/05/2021

Kocha wa zamani wa Chelsea Frank Lampard ndiye anayeoneka kuwa mtu sahihi wa kuchukua nafasi ya Roy Hodgson katika klabu ya Crystal Palace. Mkataba wa Hodgson ambaye pia ni kocha waw zamani wa England unamalizika mwisho wa msimu huu. (Telegraph)


Afisa mkuu mtendaji wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke amesema mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 20 , atasalia katika klabu hiyo msimu ujao. (ESPN, via Bild)

Barcelona wamewasiliana na wawakilishi wa kocha wa Bayern Munich Hansi Flick, huu kukiwa na mashaka juu ya mustakabali wa hatma ya kocha wa sasa Ronald Koeman katika klabu hiyo. (ESPN)

 


Barcelona wamefanya mawasiliano na golikipa wa Juventus Mkongwe Gianluigi Buffon, ambae ataachana na vibibi vizee hao wa Turin, mwishoni mwa msimu (Foot Mercato - in French)

Afisa mkuu mtendaji ajaye wa Bayern Munich Oliver Kahn ametaja hatua yoyote ya uhamisho wa Haaland ni "isiyofikirika" kwa sababu ya ada ya zaidi ya euro millioni 100 sawa na (£85m) ambayo inazungumziwa. (Goal, via Bild)

Winga wa Dortmund na England Jadon Sancho, 21, anamshinikiza wakala wake kufanikisha uhamisho wake kwenda Manchester United baada uhaimisho huo kugonga mwamba msimu uliopita. (Manchester Evening News)

Manchester United wanavutiwa na mlinzi wa Atalanta Muargentina Cristian Romero, 23, ambaye ameungana na mlinzi wa Lille aliye na umri wa miaka 21- Mholanzi Sven Botman na mchezaji wa Sevilla Jules Kounde, 22 , katika orodha ya wachezaji wanaosakwa na klabu hiyo ya Ligi ya Primia. (Sky Sports)

Kocha wa zamani wa Bournemouth Eddie Howe amekubali kuwa meneja mpya wa Celtic. (TalkSport)

Tottenham wanajiandaa kuanza usaili wa kumtafuta kocha mpya katika kipindi cha siku chache zijazo. Scott Parker wa Fulham ameorodheshwa lakini klabu hiyo haijakata tamaa ya kumpata meneja wa Leicester City, Brendan Rodgers. (Football Insider)

Mshambuliaji wa Slavia Prague aliye na umri wa miaka 19-raia wa Senegal Abdallah Sima, ambaye ananyatiwa na Arsenal na West Ham, anapania kuhamia Ligi ya Premia. (Standard)

Mchambuzi wa soka wa Ian Wright anamshauri kiungo wa kati wa Brighton na Mali Yves Bissouma, 24, kutokubali kujiunga na Liverpool na badala yake akubali ofa ya kujiunga na Manchester United msimu huu wa joto. (Metro)

Kiungo wa kati wa Rennes Mfaransa Eduardo Camavinga, 18, "anasakwa klabu kadhaa kubwa" kwa mujibu wa wakala wake Jonathan Barnett, ambaye pia anamwakilisha Gareth Bale. (Goal)

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta anahitaji kufanya usajili wa mabeki wawili, kiungo wa kati, mshambulizi pamoja na kipa msimu ujao ili kuijenga upya Arsenal (Goal)

Gunners wanamtaka kiungo wa kati wa Sheffield United Sander Berge na wamewaomba wasaka vipaji kuanza mchakato wa kumtafuta kiungo wa kati wa Norway ally na umri wa miaka 23. (Yorkshire Live)

Mshambuliaji wa Manchester City na Ujerumani Lukas Nmecha, 22, ananyatiwa na klabu za Ligi ya Premia na Bundesliga kwa mujibu wa baba yake baada ya kuonesha umahiri mkubwa msimu huu katika klabu ya Anderlecht, ambako alifunga mabao 18 katika mechi 37. (The Boot Room)

Tottenham wamebadili mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Newcastle Muingereza Bobby Clark, 18, ambaye ni mtoto wa kiume wa Lee Clark. (Football Insider)

Ligi ya England inajiandaa kuingia mkataba wa miaka mitatu wa haki ya kurusha matangazo na kampuni ya Sky Sports, BT Sport na Amazon Prime utakaodumu mpaka 2025 na ukiwa na thamani ya £4.5b. (Mirror)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...