Kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte, ambaye ameachana na klabu ya Inter Milan jumatano wiki hii anataka kujiunga na klabu ya Tottenham. (Guardian)
Japo Tottenham wanaangalia uwezekano wa kumuajiri Conte, lakini pia wanaweza kumuwinda Zidane. (Telegraph)
Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anajiandaa kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu na klabu hiyo yenye maskani yake katika dimba la Old Trafford, licha ya United kupoteza mechi ya fainali ya kombe la dhidi ya Villarreal. (Telegraph - subscription required)
Solskjaer anapanga kusajili wachezaji watatu kama kipaumbele chake katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. Wachezaji hao ni mlinzi wa Villarreal Pau Torres, 24, pamoja na wachezaji watatu wa timu ya taifa ya England ambao ni kiungo wa West Ham Declan Rice, 22, winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 21, na mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 27. (Guardian)
Klabu ya Juventus inatarajiwa kumfuta kazi kocha wao Andrea Pirlo na kumrejesha kocha wao wa zamani Massimiliano Allegri. (Guardian)
Allegri anaweza kusaini mkataba na Juventus ndani ya saa 24 zijazo. (Sky Sports)
Klabu ya Real Madrid ilikuwa ikimpigia hesabu Allegri kuchukua nafasi ya Zinedine Zidane, ambaye amejiuzulu kuinoa klabu hiyo jana Alhamisi. Madrid sasa wanatarajiwa kuhamishia nguvu zao katika kumsaka kocha wa PSG Paris St-Germain manager Mauricio Pochettino. (Goal)
Simone Inzaghi anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha wa Inter Milan baada ya kuachana na klabu ya Lazio. (Athletic - subscription required)
Kocha wa zamani wa Tottenham Jose Mourinho anataka kiungo wa Uswizi na Arsenal Granit Xhaka, 28, kuwa mchezaji wa kwanza kumsajili katika klabu ya Roma. (Sky Italy, via Metro)
Arsenal wanatazamiwa kutaka kulipwa dau la pauni milioni 21.5 kwa ajili ya Xhaka - lakini Roma wanaamini watalipa kitita kisichozidi pauni milioni 10. (Sky Sports)
Kumfuta kazi kocha Ronald Koeman kutawagharimu Barcelona takribani pauni milioni 12. (RAC1 - in Spanish)

No comments:
Post a Comment