Kocha Zinedine Zidane ameamua kuondoka Real Madrid na tayari ameshawafahamisha wachezaji juu ya uamuzi wake siku ya Jumatano . (AS - in Spanish)
Leicester City wanakaribia kukamilisha makubaliano ya usajili wa pauni milioni 18 wa kiungo wa mabingwa wa Ligi ya Ufaransa Lille, Boubakary Soumare, 22. (Sky Sports)
Leicester pia wanaweza kumpa nafasi ya kusalia katika Ligi ya Premia beki wa kati wa klabu ya Schalke Mturuki Ozan Kabak, 21 - ambaye amekuwa Liverpool kwa mkopo kwa nusu ya msimu uliokamilika. (Mirror)
Borussia Dortmund inafanya mawasiliano na Chelsea juu ya uwezekano wa kuwasajili Tammy Abraham, 23, na Callum Hudson-Odoi, 20. (90min)
Hatua hiyo inakuja kama pigo kwa West Ham, ambao huenda wasiweze kufikia kiwango cha pauni milioni 40 ambacho Chelsea wanakitaka kwa ajili ya Abraham. (TeamTalk)
Wakati huo huo, nia ya Dortmund ya kumtaka Hudson-Odoi inaweza kutoa fursa kwa mshambuliaji wa England Jadon Sancho, 21, kuondoka katika klabu ya Bundesliga kuelekea Manchester United. (Mirror)
Liverpool wamefikia makubaliano ya kumsajili beki Mfaransa Ibrahima Konate, 22, kutoka klabu ya RB Leipzig kwa mkataba wa miaka mitano. (ESPN)
Matumaini ya Livepool kumsajili kiungo wa Udinese Muargentina Rodrigo de Paul mwenye umri wa miaka 27 yameongezeka baada ya AC Milan kuachana na mpango wa kutaka kumsajili. (Express)
Winga wa Brazili Raphinha, 24, anasema kuwa hafikirii kuhusu kuondoka Leeds United, licha ya tetesi zinazomuhusisha na kuhamia katika klabu za Manchester United na Liverpool. (Metro)
Klabu za Primia Ligi zitatakiwa kusubiri hadi Julai kabla ya kuwasiliana na Barcelona kuhusu mipango ya kumsajili mshambuliaji Mbrazili Philippe Coutinho, 28. Arsenal na Everton wanadhaniwa kuwa
Mlinda mlango Muingereza Sam Johnstone, 28, anasema mustakabali wake upo mikononi mwa klabu ya West Brom licha ya kuhusishwa na taarifa za kuhamia Leeds na West Ham kwa malipo ya pauni milioni 20. (i paper)
Meneja wa Lazio Simone Inzaghi anaweza kuchukua nafasi ya Antonio Conte kuinoa klabu bingwa wa Ligi ya Italia Inter Milan. Conte ameammua kuondoka Inter kwa kuwa uongozi wa klabu hiyo unataka kuucha wachezaji wenye thamani ya euro milioni 80 ili kukabiliana na ukata wa kifedha. (Sky Sports)

No comments:
Post a Comment