Winga wa Brazil Willian anatarajiwa kuondoka Arsenal mwisho wa msimu huu , lakini The Gunners haijapokea maombi yoyote ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32. (Fabrizio Romano, via Mail
Kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans atafanya mazungumzo ya kandarasi mpya na Leicester mwisho wa msimu huu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye alifunga goli la ushindi la Foxes katika fainali ya FA dhidi ya Chelsea , ana miaka miwili iliosalia katika kandarasi yake. (Mail)
Aliyekuwa mkufunzi wa Juventus Massimiliano Allegri anaonekana kuwa kipaumbele katika kuchukua mahala pake mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane badala ya aliyekuwa mshambulia hatari wa timu hiyo Raul kuwa mkufunzi mpya wa klabu hiyo. (Marca)
Barcelona imeanza mazungumzo na kiungo wa kati wa zamani wa klabu hiyo ambaye kwa sasa anaifuynza klabu ya Al Saad ya Qatari Xavi kuchukua mahala pake Ronald Koeman kama mkufunzi mpya wa klabu hiyo ya NouCamp.. (ARA Esports, via Football Transfers)
Ronald Koeman
Beki wa Netherlands Sven Botman, ambaye alihusishwa na uhamisho wa kuelekea Liverpool mwezi Januari , anasema kwamba ligi ya Premia ina kitu maalum , lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 aliongezea kwamba anafurahia kwa sasa katika klabu hiyo ya Ufaransa.. (Athletic - subscription required)
Beki wa Tottenham Toby Alderweireld analengwa na klabu ya Ubelgiji Club Bruges lakini mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ubelgiji hatafanya uamuzi kuhusu hatma yake hadi atakapojua ni nani atakayechukua ukufunzi wa klabu hiyo kutoka kwa kaimu meneja wa Spurs Ryan Mason. (Voetbal 24, via Express)
Leeds United na Burnley wamejiunga na klabu ya Southampton, Watford na Rangers katika kutaka kumsaini winga wa Newcastle Jacob Murphy, 26. (Football Insider)
Jacob Murphy
Crystal Palace inatumai kumsaini beki wa Romania mwenye umri wa miaka 19 Radu Dragusin kwa mkopo kutoka kwa klabu ya Juventus nchini Itali. (Sun)
Kiungo wa kati wa Uturuki Hakan Calhanoglu ambaye kandarasi yake inakamilika tarehe 30 mwezi Juni katika klabu ya AC Milan, anasema kwamba hatma yake haitegemei timu hiyo kutinga ligi ya mabingwa Ulaya na kwamba atajadli hali yake nao mwisho wa msimu huu. (Sky Sport Italia, via Football Italia)
Hakan Calhanoglu
Mkurugenzi wa klabu ya Sasuolo Giovanni Carnevali anasema kwamba haiwezekani kabisa kwamba kiungo wa kati wa Itali, Manuel Locateli atasalia katika klabu hiyo ya Serie A msimu ujao, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kuhusishwa na baadhi ya klabu. (Sky Sport Italia, via Football Italia)

No comments:
Post a Comment