Chelsea wako tayari kumsajili tena mshambuliaji wa Inter Milan Rumelu Lukaku msimu huu wa joto huku klabu hiyo ya Italia ikiwa imejiandaa kusikiliza ofa kwa ajili ya Mbelgiji huyo wa miaka 28 (Mail)
Manchester United wamekubaliana masharti binafsi na Jadon Sancho, 21, lakini bado hawajatoa zabuni rasmi kwa winga huyo wa Borussia Dortmund na England.(Sport 1, via Star)
Thomas Tuchel yuko karibuni kusaini mkataba mpya baada ya kuiongoza Chelsea kunyakua taji la ligi ya mabingwa, huku Mjerumani huyo akitarajiwa kupatiwa mkataba wa mpaka mwaka 2023. (Guardian)
Tottenham wanafanyia kazi uteuzi wa Antonio Conte kama kocha sambamba na Mkurugenzi wa michezo wa zamani wa Juventus Fabio Paratici kama mkurugenzi wa mchezo wa mpira . (Sport Italia, via Express)
Tottenham pia wanapanga uhamisho wa kushtukiza wa mlinzi wa Chelsea Mjerumani Antonia Rudiger, 28, ingawa wanaweza kukutana na ushindani kutoka Paris St-Germain. (Mirror)
Arsenal itapaswa kuwalipa Real Madrid kiasi cha euro milioni 60 kwa ajili ya kiungo wa kati wa Norway Martin Odegaard,22, ambaye wana mpango wa kumpa mkataba wa kudumu baada ya kucheza kwa mkopo. (Defensa Central-in Spanish)
Kiungo wa kati wa Arsenal Granit Xhaka, 28, amesema ameshawishiwa na kocha wa Roma Jose Mourinho kujiunga na klabu yake lakini ana furaha kusalia kwenye klabu ya London. (Blick, via Goal)
Mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala anajiandaa kufanya mazungumzo mapya kuhusu mkataba mpya na Juventus, huku kocha mpya Massimiliano Allegri akiwa na lengo la kumpata mchezaji huyo mwenye miaka 27 kwa mkataba wa muda mrefu baada ya kurejea Turin. (Goal)
Kiungo wa kati wa Atletico Madrid Mhispania Saul Niguez, 26, atashinikiza kuhamia Manchester United mbele ya Juventus au Paris St-Germain katika dirisha la usajili la majira ya joto (Mirror)
Kiungo wa Uholanzi Gini Wijnaldum, 30, bado hajakwenda Barcelona na anasema bado anaiaga Liverpool (ESPN Netherlands via Liverpool Echo)
Mlinzi Thiago Silva anajiandaa kusalia Chelsea kwa msimu mwingine baada ya mchezaji huyo, 36, kuisaidia timu yake kupata ushindi wa ligi ya mabingwa. (Evening Standard)
Hatua ya Arsenal kumchukua mshambuliaji wa Ureno mwenye umri wa miaka 18 wa Sporting Lisbon Tiago Tomas iko katika mizani baada ya Gunners kushindwa kufuzu Uropa. (Sun)
Mshambuliaji wa Villarreal Mhispania Gerard Moreno, 29, anazivutia West Ham, Newcastle na Roma. (Calciomercato-in Italian)
Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Tottenham Serge Aurier,28, amesema anajiandaa kuachana na klabu hiyo, msimu huu wa joto huku PSG na AC Milan zikiwa timu zinazovutiwa na mchezaji huyo. (L'Equipe)
Watford wanataka kumsajili mshambuliaji Eddie Nketiah , lakini Arsenal wanataka pauni milioni 15 kwa ajili ya Muingereza huyo, ambaye amebakisha mwaka mmoja wa mkataba wake na Arsenal (Sun)

No comments:
Post a Comment