NA THABIT MADAI,ZANZIBAR
KATIBU wa kamati ya Amani Zanzibar, Fadhil Suleiman Soraga, amesema Zanzibar kuwepo kwa kamati hiyo imesaidia Zanzibar kuendelea kuwepo kwa amani na utulivu hasa katika kipindi cha siasa katika Uchaguzi Mkuu uliomalizika hivi karibuni.
Akizungumza katika mafunzo ya siku tano kwa wadau wa amani kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki ikiwemo, Sudani ya Kusini, Egpyt, Sudan, Uganda,Egypti,Kenya, Burundi na Zanzibar mafunzo ambayo yalifanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Blue bay beach resort Kiwengwa Mkoa wa kaskazini Unguja.
Alisema mara nyingi kipindi cha uchaguzi Zanzibar kunaviashiria vya kuwepo michafuko ambapo wananchi wengi wamekuwa wakiishi kwa hofu ila kuwepo kwa kamati hiyo imesaidia kwani viongozi wa dini wamesaidia kwa kiasi kikubwa kuendelea kuwaelimisha waumini wao.
Aidha alisema, kuwepo kwa mradi huo kumewasaidia waislamu wa dini za kiislamu na kikiristo kushirikiana na kufanya mambo yao pamoja kwani wamek.
Alisema tangu kuanza kwa mradi huo waumini hao wamekuwa wakifanya mambo ya maendeleo kwa mashirikiano ya kufanya kazi ya kuhubiri amani na upendo kwa jamii juu ya umuhimu wa amani na upendo bila kubaguana kwa misingi ya dini.
Katibu Mkuu wa Umoja ya majimbo ya Kanisa Anglikana Barani Afrika, Decrafti Johnson Kofi, aliiomba serikali kuendelea kuunga mkono mradi huo kwani umeleta manufaa kwa waislamu wa dini tofauti pamoja na kuwaunganisha pamoja.
Aidha alisema kupitia mafunzo yanayotolewa kupitia mradi huo kwa viongozi wa dini umeweza kuwaunganisha na kuacha tofauti zilizokuwa zikijitokeza kwa waumini wao.
Mapema Meneja Mradi wa amani Zanzibar, Jamal Ali Hussein, alisema, alisema mradi huo unaendeshwa kupitia umoja wa Ulaya unaoendesha mradi wa kuendeleza amani kupitia kamati ya viongozi wa dini wenye lengo la kuondosha kisiasa za mifarakano kupitia dini.
Alisema kupitia nkamati hiyo, waliweza kuandaa utaratibu wa kuwakutanisha viongozi wa dini zote katika harakati za maendeleo kwa kuona wananchi wa Zanzibar wanaondokana na mifarakano iliyokuwa inajitokeza katika kila kipindi cha kabla na baada ya uchaguzi mkuuu unaofanyika kila baada ya miaka mitano visiwani hapa.
“Katika mwaka 2020 hali ya kisiasa Zanzibar ilikuwa shuwari haikutokea mifarakano ya kidini wala kisiasa pamoja na kubaguwana kwa waumini wa dini za kiislamu na kikiristo kwa tofauti za dini”, alisema,
Hata hivyo Meneja huyo alisema kutokana na kuendelea kwa mradi huo watahakikisha wanaondoa mifarakano ya kisiasa ndani ya jamii ambayo ilikuwa ikileta ubaguzi.
Sambamba na hayo Meneja huyo aliwataka waumini wa dini zote (Kiislamu na kikiristo) kuendeleza umoja uliokuwepo kati yao na kuondosha tofauti zao za kisiasa.
“Mradi huo pia umeondosha fujo tofauti ambazo zilikuwa zinajitokeza baina ya vyama vya siasa na dini zetu”, alisema.
Hata hivyo aliwashukuru waandishi wa habari kwa kuelimisha wananchi juu ya suala zima la amani na kuwataka kutokuwa chanzo cha kuhatarisha amani na utulivu uliopo.
Waunde kamati za amani masheikh nmufti na wachungaji katika ngazi za mikoa na wilaya kitaifa.
Aliwataka viongozi wa dini kudini na akaepamoja kusimamia imani katika mahubiri zao pamoja na kuwa na sheria katika kuzungumza lugha moja katika kuendeleza amani.
Mradi wa kuendeleza amani (CRID) umefadhiliwa na umoja wa ulaya kwa kushirikiana na serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
No comments:
Post a Comment