Search This Blog

Tuesday, May 18, 2021

Rais Joe Bide atoa wote wa kusitishwa mapigano kati ya Israel na Gaza


Washington,Rais Joe Biden wa Marekani ametoa wito wa kusitishwa mapigano kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas, wenye kulitawala eneo la Gaza, katika mazungumzo yake ya njia ya simu na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.Taarifa ya Biden imetolewa kwa uangalifu mkubwa, ikitajwa kuwa ni rai ya awamu ya pili kutolewa na Ikulu ya Marekani, kufuatia shinikizo kubwa katika kipindi ambacho mashambulizi yakiendelea.K

iongozi huyo wa Marekani ameitaka Israel pia kufanya kila linalowezekana kuwanusuru raia wasio na hatia. 

Awali Jumatatu Waziri Mkuu Netanyahu aliviambia vikosi vya usalama kwamba Israel itaendelea na mapambano hayo ambayo yamedumu kwa takribani siku 8 na kusababisha zaidi ya watu 200 kufariki dunia wengi wao wakiwa Wapalestina.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...