Na Omary Mngindo, Chalinze.
JESHI la Polisi Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani, limewaonya wananchi wenye dhamira ya kutaka kutenda makosa mbalimbali kipindi hiki cha sikukuu ya Eid, likiwataka kuacha mara moja mawazo hayo.
Limesema kuwa limejipanga kikamilifu kuhakikisha hakuna mharifu yeyote atayeweza kupata nafasi ya kufanya jambo ambalo ni kinyune cha sheria, huku likiwaomba wazazi kuwaonya watoto wao, kwani hawatokuwa na msamaha.
Mkuu wa Polisi Chalinze OCD Hussein Maro aliyasema hayo kwenye hafla ya kufuturisha, iliyoandaliwa na Mkuu huyo akishirikiana na Maofisa wenzake pamoja na wadau mbalimbali, huku mgeni rasmi akiwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete.
"Nitumie nafasi hii kuutaarifu umma kwamba jeshi tumejipanga kikamilifu kuhakikisha kipindi chote sherehe za sikukuu ya idd hakutakuwa na matukio yeyote ya uvunjifu wa amani, kwa wenye mawazo hayo waache mara moja," alisema Maro.
"Tuko imara katika maeneo yote ya Chalinze, askari wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wananchi wanasherehekea kwa amani, na kwamba yeyote atayethubutu kufanya tukio lolote atakumbana na kichapo," alisema Maro.
Kwa upande wake Ridhiwani alisema kuwa wakati Chalinze ikijiandaa kuwa Wilaya, upande wa Polisi wapo vizuri kupitia OCD m Maro, kwani majengo yameboreshwa na kuwa ya kisasa zaidi ukilinganisha na yalivyokuwa awali.
"Awali upande wa vyumba vya huku nyuma mtu ukienda kwa ajili ya kupekeka mashtaka unakutana na askari amevua shati anajipepea kwa joto mpaka inaaogopa, hilo lilitokana na hali ya joto kipindi hicho, lakini sasa raha tupu," alisema Ridhiwani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Ramadhani Possi alilipongeza heshi hilo chini ya Mkuu huyo, huku akiliomba liendelee na utekelezaji wa majukumu yake kwa wananchi, na kwamba chini yake limerejesha imani kwa wana-Chalinze.
"Sasa hivi imani kwa wana-Chalinze dhidi ya jeshi lao la Polisi imeimarika kisasi, nikupongeze sana na tukio ili la leo kutukutanisha kwa ajili ya futari inonesha ni namna gani ulivyokaribu na jamii, tunakuahidi ushirikiano katika kipindi chako chote," alisema Possi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuia ya Maimamu Chalinze Alhaj Hamisi Nassor alisema, kuwa kitendo cha OCD huyo kuandaa hiyo na kuwapatia sadaka wenye uhitaji ni kitendo kikubwa, huku akisema kina fadhira kubwa mbele ya Mwenyeezimungu.

No comments:
Post a Comment