Search This Blog

Thursday, May 6, 2021

Naibu Spika Tulia asema hakuna mbunge aliyejiandikisha kumuuliza maswali Waziri Mkuu

 


Naibu Spika wa Bunge,  Dk Tulia Ackson amesema hakuna mbunge aliyejiandikisha kuuliza maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Alhamisi Mei 6, 2021.

Dk Tulia ametoa ufafanuzi huo leo baada ya kuanza kwa kipindi cha maswali na majibu bungeni.

Ni utaratibu wa Bunge kila Alhamisi wabunge hupata nafasi ya kumuuliza waziri mkuu maswali ya papo kwa hapo kwa dakika zisizozidi 30.

Hata hivyo wakati Naibu Spika akisema hayo, ndani ya ukumbi wa bunge Majaliwa hakuwepo na haikuelezwa nani anayekaimu nafasi yake leo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...