Search This Blog

Wednesday, May 12, 2021

Mwenyekiti wa tume ya AU alaani mashambulizi dhidi ya Wapalestina

 


Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika amelaani kitendo cha vikosi vya Israel kushambulia ukanda wa Gaza na''ashambulizi mabaya'' dhidi ya waumini katika msikiti wa Al-Aqsa.

Moussa Faki Mahamat amesema vitendo vya jeshi la Israel na kuwaondoa Wapalestina kwenye makazi yao ni ukiukaji wa sheria ya kimataifa.

'' Mwenyekiti wa tume ya AU analaani mashambulizi katika ukanda wa Gaza yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 21 raia wa Palestina, na mashambulizi katika msikiti wa Al-Aqsa yaliyotekelezwa na vikosi vya usalama vya Israel dhidi ya waumini wa Palestina wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani,'' taarifa ya Umoja wa Afrika ilieleza.

Karibu watu 40 wamekufa kutokana na mashambulizi kati ya Israel na Gaza katika kipindi cha miaka kadhaa.

Jeshi la Israel linasema linawalenga wanamgambo walio Gaza yakiwa majibu ya mashambulizi ya roketi mjini Jerusalem na maeneo mengine.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...