Mwanamuziki wa Marekani ASAP Rocky ametangaza kwamba yupo katika mapenzi na mwanamuziki mwenza Rihanna.
Rapa huyo alimuelezea Rihanna kuwa penzi la Maisha yake katika mahojiano na GQ.
Uvumi kuhusu iwapo nyota hao wamekuwa katika uhusiano wa kimapenzi ulianza mapema 2013, wakati rapa huyo alipomsaidia Rihanna katika ziara yake ya Diamond World Tour.
"Yeye ni sawa na labda milioni wengine . Nadhani wakati unajua, unajua tu," alisema. "Ni Yeye tu."
Wawili hao walishiriki katika Video ya ASAP Rocky ya 2013 ya fashion Killa.
Tangu wawili hao walipoanza mahusiano ya kimapenzi , wamekuwa wakijaribu kuwazuia waandishi wa habari kuwapiga picha pamoja, taarifa hiyo ilisema.
Rapa huyo alisema kwamba mpenzi wake ndiye aliyeishawishi albamu yake mpya ambayo itamshirikisha Morrissey.
Mwaka 2019, Asap Rockey , jina lake Rakim Mayers, alipatikana na hatia ya kumshambulia mtu wakati wa vita vilivyozuka Stockholm na kupatiwa hukumu ya miaka miwili.
Kesi hiyo ilivutia hisia za kimataifa ,wakati rais wa Marekani Donald Trump wakati huo alipoingilia kati na kusema kwamba ASAP Rocky alikuwa anaonewa.

No comments:
Post a Comment