Search This Blog

Saturday, May 22, 2021

Mkuu wa majeshii Nigeria auawa kwenye ajali ya ndege


Kamanda wa ngazi ya juu katika jeshi la Nigeria Jenerali Ibrahim Attahiru amefariki dunia jana Ijumaa baada ya ndege iliyombeba kuanguka kaskazini mwa taifa hilo. 

Msemaji wa jeshi la angani wa taifa hilo amethibitisha hayo na kueleza kuwa ndege iliyombeba ilianguka karibu na uwanja wa ndege katika jimbo la Kaduna. 

Na kwamba uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha ajali hiyo. Attahiru ambaye alikuwa mkuu wa majeshi, aliteuliwa na Rais Muhammadu Buhari mwezi Januari baada ya mageuzi miongoni mwa wakuu wa kijeshi, ili kuimarisha vita dhidi ya machafuko na mashambulizi ya wanamgambo ambayo yamedumu kwa zaidi ya muongo mmoja.

 Kupitia taarifa, Rais Muhammadu Buhari ametaja ajali hiyo kuwa pigo kubwa wakati ambapo vikosi vyao vinaelekea kumaliza changamoto zinazoikumba nchi.

 Ajali hiyo inajiri miezi mitatu tu baada ya ndege nyingine ndogo ya kijeshi pia kuanguka nje ya uwanja wa ndege wa Abuja kufuatia hitilafu za mitambo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...