Search This Blog

Sunday, May 30, 2021

Methew avikatisha tamaa vyama vya upinzani kukiondoa CCM madarakani, aliyekuwa katibu wa kanda aomba kujiunga na CCM


Na Ahmad Mmow, Lindi.

Itakuwa ni ndoto kwa vyama vya siasa nchini kukiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani.

Hayo yameelezwa leo na aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa mkoa wa Lindi na kanda ya Kusini, Selemani Methew Luwongo ( Messi). Wakati wa mkutano wa kumkabidhi rasmi kadi ya Chama Cha Mapinduzi ambao umefanyika katika kata ya Majengo, halmashauri ya Mtama wilaya ya Lindi.

Messi alisema kutokanana vyama vya upinzani kukosa dira inayovionesha mwelekeo sahihi itakuwa ni kama ndoto za alinacha kukiondoa CCM madarakani.

Messi ambaye kuhama kwake kumesababisha wanachama 380 wa  vyama vya upinzani katika jimbo la Mtama, hasa CHADEMA ambao wamekabidhiwa kadi kwenye mkutano huo alisema baada ya kujiunga CHADEMA na kushika madaraka mengi katika chama hicho alibaini chama hicho na vyama vingine vya upinzani  vikomekosa mwelekeo kwasababu ya kukosa dira.

" Mtu unachungulia unaona mhii! huku ninakoelekea na kwenda kuna ng'anya (tatizo). Kwahiyo ni ndoto za alinacha vyama vya upinzani kuiondoa CCM madarakani," alisema Messi.

Kwakuzingatia madai hayo, kada huyo mpya wa CCM  alitoa wito kwa wanachama wa CHADEMA waliopo katika jimbo la Mtama wajiunge na CCM. Kwani kuendelea kubaki CHADEMA ni sawa na kupoteza muda wao kwakutegemea jambo lisilowezekana kufanyika.

Licha ya sababu hiyo lakini pia alitaja sababu nyingine iliyosababisha ahamie CCM ni utendaji wa Rais Samia Suluhu Hassan. Kwani kwa utendaji wake angekosa la kumsoa iwapo angeendelea kuwa ndani ya CHADEMA.

" Tatizo ni kwamba ingawa mama anafanya vizuri na yupo safi. Lakini ukiwa upande ule hutakiwi kupongeza. Hata kukifanyika mazuri unataka kupongeza unaambiwa minya na kausha," alisema Messi.

Mbali na hayo kada huyo wa CCM ambaye katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana(2020) aligombea ubunge wa jimbo la Mtama  kupitia CHADEMA  aliweka wazi kwamba amejiunga na CCM siyo kwaajili ya kusaka madaraka.

Alisema amejiunga ili kishirikiana na makada wenzake kuimarisha na kujenga CCM katika jimbo la Mtama. Huku akibanisha kwamba anagombea wakati uchaguzi mkuu umepita.

Katika hatua nyingine aliyewahi kuwa katibu wa  CHADEMA kanda ya   Kusini, Filbert Ngatunga alitumia mkutano huo kujiunga na CCM. Ombi ambalo limekubaliwa na mgeni rasmi katika mkutano huo ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa    Chama Cha Mapinduzi(UVCCM),  Heri James.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...