Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu wa Kilabu ya Crystal Palace inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL) na Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa amekubali ombi la Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuwa Balozi wa hiyari wa utalii wa Tanzania.
Mamadou Mamadou Sakho amekubali ombi hili wakati alipokutana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Betrita Lyimo katika Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.
Mamadou Sakho amekuwa Tanzania kwa ziara ya mapumziko pamoja na familia yakeImage caption: Mamadou Sakho amekuwa Tanzania kwa ziara ya mapumziko pamoja na familia yake
Mamadou ambaye ni raia wa Ufaransa amekuwa nchini Tanzania tarehe kwa mapumziko ya siku 10 akiwa ameambatana na familia yake ambapo alitemebelea maeneo ya utalii nchini humo ikiwa ni pamoja na Hifadhi ya wanyama ya Serengeti.

No comments:
Post a Comment