Search This Blog

Sunday, May 16, 2021

Mapigano yaanza tena Afghanistan baada ya kusitishwa kwa siku tatu

 


Mapigano kati ya Taliban na vikosi vya serikali ya Afghanistan yameanza tena mapema leo asubuhi katika jimbo la Helmand, baada ya kumalizika kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kwa siku tatu. Makubaliano hayo yalifikiwa ili pande zote zinazohasimiana ziweze kusherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr.


Msemaji wa jeshi la Afghanistan na afisa wa eneo hilo wamesema kulikuwa na mapigano kwenye viunga vya Lashkar Gah, mji mkuu wa Helmand, ambao umeshuhudia mapigano yakiongezeka tangu Marekani ilipoanza kuyaondoa majeshi yake Afghanistan kuanzia tarehe moja ya mwezi huu wa Mei. Aidha, msemaji wa Taliban, Zabihullah Mujahid amesema vikosi vya serikali ya Afghanistan ndiyo vimeanzisha operesheni, hivyo kundi hilo lisilaumiwe. 


Makubaliano ya kusitisha mapigano kwa siku tatu yaliyoanzishwa na Taliban na kukubaliwa na serikali ya Afghanistan, yalimalizika jana usiku.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...