Search This Blog

Wednesday, May 5, 2021

Mahindi yaliyokwama mpakani yaruhusiwe kuingia nchini - Rais Kenyatta

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amemuagiza waziri wake wa biashara kuondoa msongamano wa bidhaa katika mipaka ya Kenya na Tanzania.

Bw. Kenyatta ametoa muda wa wiki mbili mahindi yote yaliyokwama mpakani kuruhusiwa kuingia nchini.

''Hiyo mahindi imelala hapo mpakani,Waziri mimi nakupatia wiki mbili…yote ifunguliwe na hiyo maneno iishe'' alisema.

Kenyata ametoa tamko hilo leo mbele ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wakati wa kongamano la wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya linaloendelea jijini Nairobi.

Mapema mwezi Machi Kenya ilipiga marufuku ununuzi wa mahindi kutoka mataifa jirani ya Tanzania na Uganda.

Uamuzi huo ulifikiwa baada ya uchunguzi kubaini kwamba mahindi kutoka mataifa hayo mawili sio salama kwa matumizi ya chakula cha binadamu.


 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...