Search This Blog

Tuesday, May 25, 2021

Mahakama ya ICC yaanza kusikiliza kesi ya ukatili wa Darfur


Kesi inayomkabili mbabe wa kivita anayeshitakiwa kwa uhalifu wa kivita katika mkoa wa Darfur nchini Sudan, imeanza kusikilizwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC, ikiwa ni takribani miaka 15 tangu uchunguzi dhidi ya ukatili huo ulipoanza. 

Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya ICC Fatou Bensouda amesema kuwa, Ali Muhammad Ali Abd-al-Rahman anatuhumiwa kwa mauaji, ubakaji na mateso katika matukio 13 yanayohusiana na mapigano ya kikabila yaliyoukumba mkoa wa Darfur miongo miwili iliyopita. 

Abd-al-Rahman ambaye pia anajulikana kama Ali Kushayb, alijisalimisha mwenyewe katika mahakama hiyo mwaka uliopita.

 Alikuwa ni miongoni mwa viongozi wakuu katika kundi la wanamgambo la Janjaweed lililoendesha operesheni zake mjini Darfur kati ya mwaka 2003 na 2006 na kuhusika na vifo vya watu 300,000.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...