Search This Blog

Tuesday, May 18, 2021

Maelfu ya watu wahama makaazi yao kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua nchini Burundi


Karibu watu elfu 5 waliachwa bila makaazi nchini Burundi kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua nyingi zilizonyesha.

Kutokana na mvua za masika zilizonyesha magharibi mwa Burundi, mito ya Rusizi, Mpanda na Kajeke ilifurika na kusababisha mafuriko.

Katika taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Burundi, ilielezwa kuwa nyumba, barabara na ardhi katika makaazi ya karibu na mito zilifurika maji na karibu watu elfu 5 walilazimika kuhama.

Kwa ushirikiano wa serikali na Shirika la Msalaba Mwekundu la Burundi, mahema yaliwekwa kwa ajili ya kutoa hifadhi kwa waathirika wasio na makaazi.

Wataalam wa utabiri wa hali ya hewa walitangaza kuwa maji ya mito yaliongezeka na mafuriko yalitokea kwa sababu ya mvua isiyo ya msimu. Wataalam pia walionya kuwa mvua hizo zitaendelea kunyesha katika siku zijazo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...