Search This Blog

Thursday, May 13, 2021

Madiwani Rorya waomba kushirikishwa kwenye miradi

 


Na Timothy Itembe, Mara.

Madiwni katika halmashauri ya Rorya mkoani Mara wameomba kushirikishwa kwenye ukusanyaji wa mapato ili kuchochea kupanda kwa makusanyo.

Akiongea kwa niaba ya wenzake diwani kata ya Roche,Jumanne Ally Oketho ndani ya baraza la madiwani lililokaa ukumbi wa SOA alisema ili makusanyo kupanda kuna haja madiwani kushirikishwa katika swala zima la ukusanyaji wa mapato.

Diwani huyo pia alitumia nafasi hiyo kuwatupia lawama watendaji ambao wa vijiji na kata ambao  wanakwamisha jitihada za madiwani kutaka kushiriki huku wakijua  makusanyo ya mapato ndani ya halmashauri pamoja na maeneo husika.

“Mimi niombe baraza lako mwenyekiti kuidhinisha sheria ya madiwani kushirikishwa katika swala zima la ukusanyaji mapato kutoka maeneo yetu bila watumshi kutuwekea mikingamo ya pingamizi na kufanya hivyo itasaidia makusanyo ya halmashauri  kupanda kwa utekelezaji wa miradi”alisema Oketho.

Oketho alimaliza kwa kusema kuna baadhi ya watendaji wa kata na vijiji wanakwamisha jitihada za madiwani kushiriki katika maeneo ambayo makusanyo yanaendelea licha ya kuwa maeneo hayo ni moja ya utawala wa diwani husika.

Kwa upande wake diwani kata ya Nyamtinga,Syluana Didacus Ndemera alisema kuna baadhi ya watendaji wa vijiji na kata wanatumia nafasi hiyo kuwatoza kodi mara mbili wafanyabiashara jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu.

Diwani huyo alitolea mfano wafanyabiashara wa Samaki kuwa wanatozwa mara mbili kodi pindi wanapokutwa na wakusanyaji wa ushuru barabarani bila kujali kuwa wafanyabiashara hao wamelipa ushuru kutoka maeneo waliochukulia mzigo.

Ndemera aliomba halmashauri yake kutafuta makusanyo ya ushuru rafiki kutoka kwa wafanyabiashara ili kila mfanyabiashara alipe kodi na ushuru wa halmashauri kulingana na mapato ya mtaji na faida anayo pata vinginevyo wafanyabiashara watafirisiwa mtaji na kushindwa katika swala zima la kuchangia shuguli za maendeleo ikiwemo ya kuendesha maisha ya kifamilia.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Gerald Ng’ong’a aliomba halmashauri yake kuzingatia maamuzi ya baraza kwa usitawi wa halmashauri pamoja na wananchi kwa ujumla.

Ong’ong’a pia aliomba madiwani kuibua miradi pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kupata fedha nyingi katika halmashauri hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi kwa jamii.

Mwenyekiti huyo alitumia nafasi hiyo kuomba miradi yote iliyo kwenye mpango itekelezwe kwa kuzingatia BOQ huku watumishi na madiwani wakishirikiana kwa kuijenga Rorya sio vinginevyo.

Naye mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Charles Chacha alipongeza madiwani na kuomba ushirikiano katika kutekeleza miradi kwa wanarorya ili kunufaika na halmashauri yao.

Chacha alitumia nafasi hiyo kuwataka madiwani wenye hoja kufika ofisini kwake ili kujadili na kuzitafutia ufumbuzi hoja huku wakiacha kulalamika malalamiko yasioyokuwa na sababu za msingi.

Mkurugenzi huyo alifungua milango kwa wale ambao wanataka kuingia Ofisini kwake kufika kwa masilahi mapana ya halmashauri bila kusita na alitumia nafasi hiyo  kuonya wenye utengano  unaoweza kuzua maswala yasiyokuwa na hoja za misingi ya kujenga Rorya kwa maendeleo na kuwa kinachotakiwa ni kujali utekelezaji wa maendeleo kwa kuzingatia sheria na taratibu pamoja na kanununi zilizopo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...