Bangladesh ilitenga karantini kambi tano za wakimbizi wa Arakan zilizoko katika jiji la Cox's Bazar kusini mwa nchi kwa sababu ya kuongezeka kwa kesi za maambukizi ya virusi vya corona (Covid-19).
Kulingana na taarifa ya Al Jazeera, Mwenyekiti wa Tume ya Msaada wa Wakimbizi ya Bangladesh, Shah Ridhwan Hayat, alisema kuwa karantini hiyo itaendelea hadi Mei 27.
Katika muktadha huu, wakati kuingia na kutoka kambini ni marufuku, hatua zitachukuliwa kupunguza ujumuikaji baina ya watu ndani ya kambi hizo.
Mratibu wa afya wa eneo hilo Toha Bhuiyan alitangaza kuwa wakimbizi 45 kati ya 247 walifanyiwa vipimo siku iliyopita na kukutwa na Covid-19, na idadi hiyo hiyo ya kesi za maambukizi pia ziligunduliwa jana.
Hadi kufikia sasa, watu 13 wamepoteza maisha na kesi 863 za maambukizi zimegundulika katika kambi 34 ambapo takriban wakimbizi milioni 1 wa Arakan wanaishi baada ya kutoroka Myanmar kutokana na mashambulizi ya jeshi na Wabudhi washupavu.

No comments:
Post a Comment