Jaji Mkuu wa Iran aliyewahi kugombea kiti cha urais hapo nyuma Ebrahim Raisi, ametangaza leo Jumamosi kugombea tena kiti hicho katika uchaguzi mkuu mwezi Ujao, hii ikiwa ni kulingana na taarifa kutoka kwa chombo kimoja cha habari nchini humo.
Jaji huyo wa zamani alikuwa hasimu mkubwa wa rais Hassan Rouhani katika uchaguzi wa mwaka 2017 na kulikuwa na fununu kupitia vyombo vya habari kuwa huenda atagombea mwaka huu. Katika taarifa yake, Raisi amesema ameamua kugombea kutokana na matakwa ya wengi na ana nia ya kugombea kupitia chama binafsi ili alete mabadiliko katika utendaji na namna ya kuiendesha nchi.
Pia ameahidi kupambana na Umasikini, rushwa, udhalilishwaji pamoja na ubaguzi iwapo atachaguliwa, na hizi ndizo zilizokuwa ahadi zake miaka minne iliyopita wakati akigombea nafasi hiyo ya juu katika Jamhuri hiyo ya kiislamu.
Katiba ya Iran inamzuia Rais wa sasa Hassan Rouhani kugombea muhula mwengine wa tatu madarakani.

No comments:
Post a Comment