Israel imeendelea na mashambulizi ya anga dhidi ya Ukanda wa Gaza hivi leo, huku ikisema bado haijatuma wanajeshi yake wa ardhini kwenye vita hivyo vilivyoanza Jumatatu.
Wanamgambo wa Hamas nao wameendelea kurusha makombora yao kuelekea Israel, huku mzozo huo ukiwa umeshababisha zaidi ya vifo vya watu 100 kwa upande wa Wapalestina. Makombora yaliyorushwa jana usiku na Hamas yalifika hadi karibu na uwanja wa ndege wa Ben Gurion uliopo Tel Aviv, na pia kwenye miji ya pwani ya Ashdod na Ashkelon.
Jioni ya jana, jeshi la Israel liliripoti pia kurushwa kwa makombora yaliyotokea upande wa Lebanon, ingawa lilisema hakukuwa na madhara yoyote. Ndani ya Israel kwenyewe, makabiliano ya mitaani baina ya Mayahudi na Waarabu yameripotiwa

No comments:
Post a Comment