Search This Blog

Thursday, May 13, 2021

Iran yasema iko tayari kuzungumza na Saudi Arabia

 


Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran, Mohammad Javad Zarif, amesema kwamba nchi yake ipo tayari kujenga mahusiano ya karibu na hasimu wake, Saudi Arabia. 

Akizungumza baada ya mkutano wake na Rais Bashar al-Assad wa Syria mjini Damascus, Zarif alisema tayari Iran imeshaanza mawasiliano na Saudia. 

Aliliambia shirika la habari la Syria, SANA, kwamba wanatazamia mawasiliano hayo yatapelekea mashirikiano makubwa kati ya mataifa hayo mawili, ili ipatikane amani na utulivu kwenye kanda nzima ya Ghuba, hasa kwa taifa la Yemen, lililoharibiwa vibaya kwa vita. 

Kauli ya Zarif inafuatia matamshi ya hivi karibuni ya Mrithi wa Kiti ya Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, aliyesema nchi yake inataka kujenga uhusiano mwema na Iran. 

Saudi Arabia inayofuata madhehebu ya Sunni na Iran inayofuata madhehebu ya Shia zinaangaliana kama mahasimu wakubwa wa Ghuba, na kwa miongo kadhaa zimekuwa na ushindani unaovuka mipaka ya mataifa yao. 

Zote mbili zinahusika na vita vya Yemen, huku kila upande ukiunga mkono kundi hasimu.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...