Search This Blog

Wednesday, May 26, 2021

IKOLTO yawapa mbinu wakulima wa Mpunga Magugu kuwa na Kilimo Endelevu.


Na John Walter-Manyara

Shirika lisilo la Kiserekali, la Rikolto la Ubelgiji limefanikiwa kurudisha Mbegu bora ya mchele unaolimwa Magugu wilayani Babati mkoani Manyara kwa kuzifanyia utafiti na kupata sababu iliyofanya mchele wa Magugu kukosa sifa na soko.

Akiongea na wakulima kwenye warsha iliyoandaliwa mahsusi kwa wakulima wa mpunga wa Kata ya Magugu ambao ndiyo wahusika wakuu, mshauri wa kilimo Biashara Bi Djalou Franco alisema shirika hilo kupitia wataalam wamefanya kazi kubwa kuhakikisha mbegu ya asili ya Magugu inarejeshwa.

Pamoja na jitihada za kurudisha mbegu ya asili ya mchele bora wa Magugu, wakulima pia wamefundishwa mpango wa (KILIMO ENDELEVU) cha mpunga kinachojali utunzaji wa mazingira nakuweza kumudu athari ya mabadiliko ya Tabianchi.

Kutokana na mafanikio hayo ya kurudisha mbegu hiyo kwa msimu huu wa mwaka 2021, tayari tani 18 za mbegu zimeandaliwa kwa ajili ya kilimo cha msimu wa mwaka 2022.

 Kwa upande wa afisa kilimo mkoa wa Manyara Samwel Dahay amesema wameeendelea kuboresha mazingira ya kilimo kupitia wadau mbalimbali wakiwemo Rikolto ambao wamehusika kuwajengea uwezo wakulima wa mpunga kurudi na kufufua mbegu halisi ya Magugu.

Joan Frank kutoka kampuni ya Mamba Rafiki anasema baada ya mafunzo hayo kuotoka Rikolto wanatarajia kufanya vizuri na kuongeza thamani katika mazao kwani awali walikuwa hawajui namna ya kutumia mbegu halisi ya Magugu hali iliyokuwa inatusababishia kuwa na mchele usio asili ya Magugu.

Akiongea kwenye warsha hiyo,mtafiti wa zao la mpunga kutoka TARI-IFAKARA Bw. Theodory Kessy alisema walifanya utafiti wa kilichoharibu ubora wa mchele wa magugu na kubaini baadhi ya visababishi ,likiwemo la kuchanganya mbegu, kukoboa kwa kutumia vinu visivyo sahihi na walanguzi kuhamisha mpunga kutoka maeneo mengine na kuukobolea Magugu kufuata soko la Magugu.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...