Search This Blog

Saturday, May 15, 2021

EC yatoa neno uchaguzi jimbo la Muhambwe


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage, amewataka watendaji wa uchaguzi mdogo wa jimbo la Muhambwe mkoani Kgoma kufanya kazi kwa weledi, kuzingatia sheria za uchaguzi, kanuni na maelekezo ya Tume.

Rai hiyo ameitoa alipotembelea na kukagua maandalizi ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Muhambwe ambapo pia utafanyika sambamba na ule wa jimbo la Buhigwe na kueleza kuridhishwa na maandalizi ya uchaguzi huo.

Uchaguzi huo mdogo wa majimbo hayo mawili, unafanyika kufuatia aliyekuwa mbunge wa jimbo la Buhigwe Dkt. Philip Mpango, kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais na wa jimbo la Muhambwe Mhandisi Atashasta Nditiye kufariki dunia.

Na uchaguzi huo utafanyika kesho Mei 16, 2021.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...