Search This Blog

Friday, May 14, 2021

Dk. Mpango atembelea kaburi la Magufuli

 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, leo amezuru kaburi la aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt. John Magufuli, mjini Chato mkoani Geita.


Dkt. Mpango amezuru kwenye kaburi hilo akiwa njiani kuelekea Kibondo, mkoani Kigoma kwa ajili ya kufunga kampeni za uchaguzi katika jimbo la Muhambwe.


Hayati Dkt. John Magufuli, alifariki dunia Machi 17, 2021, katika hospitali ya Mzena Dar es Salaam kutokana na maradhi ya moyo na alizikwa Machi 26 mwaka huu kijijini kwake Chato.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...