China imepuuza kitisho cha madhara yanayoweza kusababishwa na roketi iliyoanguka kutoka kwenye mzingo wa dunia baada ya kujiachanisha na kituo cha masuala ya anga cha China baada ya Marekani kuonya huenda ikaanguka kwenye eneo la makazi ya watu duniani.
Wataalamu wa kijeshi nchini Marekani wanataraji kwamba roketi hiyo aina ya Long March 5B itaanguka duniani kati ya Jumamosi na Jumapili, lakini wakionya ilikuwa ni vigumu kukisia itaangukia wapi na wakati gani hasa.
Hata hivyo msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa China Wang Wenbin amesema uwezekano wa kusababisha madhara ni mdogo mno.
Amesema kwa kiasi kikubwa roketi hiyo itaharibika itakapokuwa ikianguka na kwamba mamlaka zitauarifu umma juu ya hali ilivyo katika wakati unaofaa.

No comments:
Post a Comment