Search This Blog

Thursday, May 6, 2021

CEO wa American Airlines afunga na Waislamu

Mkurugenzi Mkuu (CEO) wa shirika la ndege la American Airlines Doug Parker, alisema kwamba alikuwa anafunga swaum kuwahurumia wafanyikazi wake wa Kiislamu.

Katika chapisho lake kwenye Linkedin, Parker alitangaza kwamba alikuwa amefunga kwa siku moja wiki iliyopita ili kujiunga na wito wa kikundi cha wafanyikazi wa Kiislamu wa shirika hilo.

Akibainisha kuwa hakula chakula wala kunywa kitu chochote kwa masaa 15, Parker alisema,

"Mwisho wa siku, nilikuwa na njaa na kiu. Hii ilinipa heshima kubwa kwa washiriki wa timu yetu ya wafanyakazi wa Kiislamu na kujitolea kwao kwa imani yao."

Chapisho hilo la Parker lilipokewa vyema kwa kupendwa na wafuasi karibu elfu 14 na kutolewa maoni zaidi ya 550 mtandaoni.


 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...