Search This Blog

Monday, May 24, 2021

Boti ya vilipuzi ya Houthis yaharibiwa


Vikosi vya muungano vinavyoongozwa na Saudi Arabia vilitangaza kuharibu boti iliyosheheni vilipuzi inayomilikiwa na kundi la Houthis linaloungwa mkono na Iran huko Yemen kusini mwa Bahari ya Shamu.

Kulingana na taarifa za shirika rasmi la Saudi Arabia la SPA, shambulizi ambalo Wahouthi walijaribu kuandaa kwa kutumia boti iliyosheheni vilipuzi katika Bahari ya Shamu lilitibuliwa..

Kulingana na ufafanuzi wa vikosi vya muungano, iligundulika kuwa wanamgambo wa Houthis wanaendelea kutishia njia za usafiri wa baharini na biashara ya ulimwengu.

Hakuna maelezo yaliyotolewa kutoka kwa kundi la Houthis juu ya suala hii.

Nchi ya Yemen ambayo imekosa utulivu wa kisiasa na kutawaliwa na mizozo kwa muda mrefu, imekuwa ikidhibitiwa na kundi la Houthis linaloungwa mkono na Iran katika mji mkuu Sana'a na maeneo kadhaa tangu Septemba 2014.

Vikosi vya muungano vinavyoongozwa na Saudi Arabia vimekuwa vikiunga mkono serikali ya Yemen dhidi ya Wahouthis tangu Machi 2015.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...