Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana kwa kikao cha hadhara siku ya Jumapili kuijadili hali inayozidi kuzorota kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Kipalestina, baada ya kufikia makubaliano na Marekani iliyozuwia mkutano huo kufanyika leo, Ijumaa.
Wanadiplomasia walisema kuwa Marekani, ambayo ni mshirika mkubwa wa Israel, awali ilitaka mkutano kwa njia ya mtandao ufanyike Jumanne. Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Antony Blinken, alisema hapo jana kwamba kusubiri kwa siku chache kungeliruhusu diplomasia kufanya kazi.
Wajumbe 15 wa Baraza la Usalamala Umoja wa Mataifa wamekutana mara mbili kwenye vikao vya ndani wiki hii, lakini hadi sasa wameshindwa kukubaliana kutoka na kauli ya pamoja, huku mapigano na uhasama kati ya Israel na Hamas ukiingia siku yake ya tano hivi leo, bila ishara yoyote ya kupunguwa.
No comments:
Post a Comment