Search This Blog

Friday, May 14, 2021

Balozi wa Israel aitaka Ujerumani kuilinda jamii ya Wayahudi

 


Balozi wa Israel nchini Ujerumani ameiomba serikali mjini Berlin kuipatia ulinzi jamii ya Wayahudi waishio Ujerumani. 


Balozi huyo, Jeremy Issacharoff ametoa rai hiyo kufuatia visa vya uhalifu dhidi ya mahekalu ya Wayahudi katika maeneo mbali mbali ya Ujerumani mnamo wiki hii. Ghasia hizo za kuwalenga Wayahudi zinadhaniwa kuwa na uhusiano na mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati baina ya Israel na Wapalestina. 


Balozi Issacharoff amesema Wayahudi wa Ujerumani hawana mchango wowote katika mzozo huo na hawapaswi kuhusishwa. Wakati huo huo msemaji wa Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema Ujerumani haitovumilia matendo yoyote ya chuki dhidi ya Wayahudi kwenye ardhi yake. 


Kauli ya Kansela Merkel imesisitizwa na rais wa shirikisho la Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier. Jumanne wiki hii, matukio ya vurugu ya kuwalenga Wayahudi yalishuhudiwa katika miji ya Munster, Duessedorf na Bonn.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...