Search This Blog

Sunday, April 25, 2021

Yanga yakubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Azam

 


AZAM FC inaayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina leo Aprili 25 imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Kipindi cha kwanza timu zote zilitoshana nguvu na kuwafanya waende vyumba vya kubadilishia nguo ubao ukisoma Yanga 0-0 Azam FC.

Ni Prince Dube dakika ya 85 alipachika bao la ushindi nje ya 18 na kumfanya afikishe jumla ya mabao 12 akiwa ni kinara kwa utupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara.

Ushindi huu unaifanya Azam FC kulipa kisasi cha kupoteza mchezo wao uliopita ambapo walifungwa bao 1-0.

Kwenye msimamo Azam FC baada ya kucheza mechi 28 inafikisha jumla ya pointi 54 ikiwa nafasi ya tatu huku Yanga ikiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 27 nafasi ya pili na kinara wa ligi ni Simba mwenye pointi 58 baada ya kucheza mechi 24.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...