Search This Blog

Tuesday, April 13, 2021

William na Harry kukutana wikiendi hii katika mazishi ya babu yao


Watawala wa Cambridge na Sussex wametoa salamu za rambi rambi kwa babu yao, mtawala wa Edinburgh aliyefariki dunia siku ya ijumaa.

Katika taarifa tofauti, Prince William alimtaja kama "mtu wa kipekee", wakati Prince Harry alisema alikuwa "mtu wa huduma" .

"Nitamkosa Babu yangu, lakini najua angependa tuendelee na kazi hiyo," William aliongeza.

Prince Philip alifariki dunia katika kasri la Windsor siku uya ijumaa akiwa na umri wa miaka 99 .

Hilo linajiri wakati mabunge kote Uingereza yalirejelea vikao vyake ili kumkumbuka mtawala huyo.

"Karne ya maisha ya babu yangu imetambuliwa na huduma - kwa nchi yake na Jumuiya ya Madola, kwa mkewe na Malkia, na kwa familia yetu," Prince William alisema katika taarifa.

"Ninajisikia mwenye bahati kuwa sio tu nilikuwa na mfano wake wa kuniongoza, lakini uwepo wake wa kudumu hata katika maisha yangu utu uzima - wakati wote mzuri na siku ngumu zaidi.

"Nitashukuru kila wakati kuwa mke wangu alikuwa na miaka mingi sana ya kumjua babu yangu na kwa wema aliomwonyesha.

"Sitawahi kuchukua kwa urahisi kumbukumbu maalum ambazo watoto wangu watakuwa nazo wakati wote wa babu yao kuja kuwachukua kwenye gari lake na kujionea hisia zake za urafiki na vile vile ucheshi wake!"

Aliongeza kuwa yeye na mkewe, Catherine, "wataendelea kufanya kile angekuwa anataka na watamuunga mkono Malkia katika miaka ijayo".

Akitoa risala za rambi rambi kwa babu yake, Prince Harry alisema: "Alikuwa kwa kweli, mwenye busara kali, na angeweza kuwasimumua watu sababu ya haiba yake - na pia kwa sababu hakujua nini atakachosema baadaye.

"Atakumbukwa kama mshirika wa kifalme aliyehudumu kwa muda mrefu mwanajeshi aliyepambwa na mataji ,mwanamfalme na mtawala mkuu'

Mazishi ya kifalme, ambayo yatapeperushwa kwa televisheni, yatafanyika kwa mtawala huyo huko St George's Chapel, katika uwanja wa Jumba la Windsor, saa 15:00 BST mnamo 17 Aprili.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...