Search This Blog

Sunday, April 11, 2021

Waziri wa ulinzi wa Marekani awasili Israel


Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amewasili nchini Israel, ikiwa ni ziara ya kwanza ya mwakilishi mwandamizi wa serikali ya Joe Biden, ambayo msimamo wake kuhusu Iran, umekuwa ukiipa mashaka serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.


Katika ziara yake hiyo ya siku mbili, Austin anatarajiwa kukutana na Netanyahu na Waziri wa Ulinzi wa Israel wa Benny Gantz, ambapo maafisa wanasema pamoja na mambo mengine mazungumzo yatajumisha mjadala kuhusu mauzo ya silaha ya Marekani kwa Israel.


Serikali ya Marekani inataka kutoa hakikisho kwa Israeli katika masuala ya usalama wa kikanda katika kipindi hiki inapoanzisha mazungumzo kwa namna tofauti, zikiwa hatua za mwanzo katika urejeaji wake kwenye makubaliano ya nyuklia ya 2015, kati ya mataifa yenye nguvu na Iran, baada ya Rais Donald Trump kuiondoa.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...