Waziri Mkuu wa Ireland Micheal Martin ameonya leo dhidi ya kurejea kwa mzozo wa makundi yanayohasimiana huko Ireland Kaskazini baada ya wiki nzima ya machafuko kwenye eneo hilo ambalo ni sehemu ya Uingereza.
Katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake, Martin amesema viongozi wa kisiasa walio madarakani hivi sasa wanayo dhima ya kuzuia kurejea kwa enzi ya giza ya mauaji na migawanyiko ya kisiasa.
Tamko lake limetolewa wakati leo Jumamosi ni maadhimisho ya mwaka wa 23 tangu kufikiwa kile kinachofahamika kama "makubaliano ya Ijumaa Kuu" yaliyomaliza miongo kadhaa ya machafuko ya Ireland Kaskazini yaliyosababisha vifo vya watu 3,500.
Polisi imesema machafuko yameendelea usiku wa Ijumaa kati ya makundi yanayopendelea Ireland Kaskazini kujiunga na Jamhuri ya Ireland na wale wanaounga mkono Ireland Kaskazini kuendelea kuwa sehemu ya Ufalme wa Uingereza

No comments:
Post a Comment