Ouhoumoudou Mahamadou ambaye aliteuliwa kama waziri mkuu nchini Niger, ameunda serikali mpya.
Serikali iliyoundwa na Mahamadou, ambaye aliteuliwa kama waziri mkuu na Rais Mohammed Bazoum mnamo Aprili 3, inajumuisha mawaziri 33.
Wakati majina kadhaa kwenye baraza la mawaziri la zamani yakihifadhi nyadhifa zao za awali, majina 22 mapya yalijiunga na serikali mpya.
Ilibainika kuwa katika serikali mpya, Mahamane Sani Mahamadou, ambaye ni mtoto wa Rais wa zamani Mahamadou Issoufou, aliteuliwa kama Waziri wa Mafuta na Nishati.
Bazoum, ambaye alishinda duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Niger mnamo Februari 21, aliapishwa kwenye hafla iliyoandaliwa katika mji mkuu wa Niamey Aprili 2 na kuanza kuhudumu rasmi.

No comments:
Post a Comment