Search This Blog

Wednesday, April 14, 2021

Watoto 20 wa shule wafa kwa ajali ya moto Niger


Takribani watoto 20 wamepoteza maisha baada ya madarasa yao kuungua moto mjini Niamey nchini Niger.

Sababu ya kuzuka kwa moto huo bado hazijafahamika.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa moto ulianzia lango la kuingilia katika shule hiyo yenye wanafunzi 800.

Moto uliosambaa katika madarasa 21 yaliyojengwa kwa nyasi , uliwanasa watoto waliokuwa ndani ya madarasa kwa kuwa hawakuwa na njia ya kutoka nje ya madarasa hayo.

"Bila kuwa na njia za dharura, wengi walinasa na wanafunzi walilazimika kupanda ukuta ili kutoroka. Wale waliokufa wengi wao ni watoto wa madarasa ya awali," Reuters ilimnukuu afisa wa chama cha walimu, Mounkaila Halidou, akisema.

Waziri Mkuu Ouhoumoudou Mahamadou ametembelea shule hiyo na kutoa salamu za rambirambi kwa wazazi wa watoto hao, Shirika la AFP limeripoti.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...