Search This Blog

Tuesday, April 20, 2021

Umoja wa Mataifa yataka uthibitisho wa UAE kuwa Bintimfalme wa Dubai yuko hai

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa nchi ya Falme za Kiarabu kutoa ushahidi thabiti kwamba Binti mfalme Latifa Al Maktoum, binti wa mtawala wa Dubai ambaye anasemekana anashikiliwa mateka, yuko hai.

Katika taarifa iliyotolewa huko Geneva Jumanne, wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa pia wamesema kuwa anastahili kuachiwa huru haraka iwezekanavyo.

Binti mfalme Latifa alijaribu kutoroka Dubai mwaka 2018. Katika video iliyoshirikishwa BBC Panorama, anasema kuwa wanajeshi walimkamata na kumrejesha alikokuwa ameshikiliwa.

Siku za nyuma, familia ya kifalme iliwahi kusema kuwa Binti mfalme Latifa yuko salama na "anatunzwa na familia yake nyumbani"

Machi 5, Umoja wa Mataifa ilisema bado inasubiri taarifa zaidi kutoka UAE - wiki mbili baada ya ombi la kwanza la kuthibitisha kuwa binti huyo yuko hai.

Katika taarifa ya Jumanne, wataalam wa Umoja wa Taifa wametoa wito kwa serikali ya UAE kwa mara nyingine tena "kutoa taarifa zenye tija" kuhusu hatma ya Binti mfalme Latifa "bila kupoteza muda"

Wametaka kupata "uthibitisho usiopendelea upande wowote juu ya hali ya msichana huyo anayeshikiliwa na kutaka aachiwe huru haraka iwezekanavyo".

"Taarifa iliyotolewa na mamlaka ya Emirates imetoa taarifa kidogo sana kuonesha kuwa anatunzwa na 'familia yake nyumbani' ambayo haitoshi," taarifa hiyo imesema.

Aliongeza: "Tuna wasiwasi kwamba baada ya video kutolewa kwa Umma mnamo mwezi Februari ambayo iliropoti kuwa Sheikha Latifa ananyimwa uhuru wake kwa kushikiliwa kinyume na hiari yake, na kufuatiwa na maombi rasmi ya kutaka taarifa zaidi kuhusiana na hali hiyo, hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na serikali."

Katika taarifa iliyopatikana na BBC Panorama mnamo mwezi Februari, Binti Latifa alisema anashkiliwa mateka katika "jumba la kifahari ambalo limebadilishwa na kuwa jela" na kwamba hapati huduma za matibabu.

Baba yake Latifa, Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, ni mmoja kati ya matajiri wakubwa duniani, mtawala wa Dubai na Makamu Rais wa UAE.

Kwa usaidizi wa rafiki zake, Latifa alisema kuwa alijaribu kutoroka Dubai kuanza maisha mapya Februari 2018.

"Siruhusiwi kuendesha gari, siruhusiwi kusafiri au kuondoka Dubai kabisa," alisema katika video iliyorekodiwa kabla tu ya kutoroka.

Lakini siku kadhaa baadaye, mwanamfalme akasema kuwa alikamatwa na wanajeshi na kusafirishwa kwa boti katika bahari Hindi. Alikamatwa na kurejeshwa Dubai ambako amekuwa akizuiliwa tangu wakati huo.

Baba yake alisema anachofanya ni kwa maslahi mema yake. Taarifa kutoka familia ya kifalme ya Dubai mwezi uliopita ilirejelea kwamba anatunzwa nyumbani.

"Sheikha Latifa anaendelea kuimarika na atajitokeza kwa umma wakati ufaao," amesema.

Kutumia simu ambayo anasema alipewa kwa siri takriban mwaka mmoja baada ya kukamatwa, binti mfalme Latifa alirekodi sauti kadhaa kwa miezi kadhaa.

Alijirekodi akiwa bafuni kwasababu huo ndio mlango pekee anaoweza kufunga. Na katika ujumbe wake ameelezea:

•alivyokabiliana na wanajeshi waliokuwa wanamrejesha Dubai kwa kutumia boti, "akiwapiga na kuwasukuma" na kumuuma mwanajeshi mmoja mkononi hadi akawa anapiga mayowe.

•Baada ya kupewa dawa za kutuliza akili, alipoteza fahamu akiwa anaingizwa kwenye ndege ya binafsi na hakuamka tena hadi ilipofika Dubai

•alikuwa anashikiliwa peke yake bila kupewa matibabu au usaidizi wa kisheria katika jumba la kifahari ambalo limefungwa madirisha na milango huku akiwa analindwa na polisi

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...