Chelsea wapo mbele ya Manchester United na Paris St-Germain katika mbio za kutaka kumsajili beki wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Raphael Varane, 28. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Beki wa Guinea Ali Camara, 23, ambaye anachezea klabu ya Young Boys ya Switzerland, amezivutia klabu kadhaa za Ligi ya Primia zikiwemo Liverpool, Arsenal, Crystal Palace, West Ham United na Norwich. (Team Talk)
Arsenal wapo njia panda juu ya mustakabali wa kiungo wao Joe Willock, 21, ambaye yupo Newcastle kwa mkopo. Arsenal wanahitaji kuuza baadhi ya wachezaji ili kujiimarisha kifedha. (Football London)
Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone ana nia ya kumsajili beki raia wa Uhispania Cesar Azpilicueta, 31, kutoka Chelsea. (El Gol Digital - in Spanish)
Manchester United na Liverpool wanaweza kujaribu kumsajili msahambuliaji machachari wa Torino na raia wa Italia Andrea Belotti, 27, ambao pia anawaniwa na vilabu vikubwa vya Italia AC Milan, Roma na Inter. Tayari Torino wanamnyemelea mshambuliaji wa klabu ya Cagliari Mbrazili Joao Pedro, 29, kama mbadala wa Belotti. (Tuttosport)
Wolverhampton Wanderers imeingia katika orodha ya klabu ambazo zinapigiwa upatu kutaka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya England, Tammy Abraham, 23. Aston Villa, West Ham na Leicester City pia wanadaiwa kutaka kumsajili mshambuliaji huyo. (Football Insider)
Kocha wa zamani wa Tottenham Harry Redknapp anategemea kuwa mshambuliaji kinara Harry Kane, 27, kuendelea kusalia katika klabu hiyo licha ya tetesi kuwa huenda akaondoka mwishoni mwa msimu.(Goal)
Manchester City wameanza majadiliano na Red Star Belgrade kwa nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji kinda wa Serbia Andrija Radulovic, 18. (Sun)

No comments:
Post a Comment