Search This Blog

Thursday, April 15, 2021

Tanzania na Marekani wafanya kazungumzo fulsa za uwekezaji hapa nchini


Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.

Mawaziri wawili wa Wizara za Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo na Wizara ya Uwekezaji Geoffrey Mwambe wamekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Donald Wright kwa lengo la kujenga ushirikiano na kushirikishana fulsa za uwekezaji zinazopatikana hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya mazungumzo hayo Waziri ya Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo amesema katika mazungumzo yao wamelenga kukuza biashara na uwekezaji baina ya nchi mbili za Tanzania na Marekani.

“Leo tumekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Donald Wright, kuona namna ya kukuza ushirikiano wetu uliopo baina ya nchi hizi mbili, bado tunafulsa nyingi na kubwa za wafanyabiashara wetu kutumia fulsa hiyo” amesema Prof. Mkumbo.

Amesema katika mazungumzo hayo wamekubaliana kuweka jitihada za kuhakikisha nchi hizo mbili zinazidi kushirikiana katika nyanja za kiuwekezaji na kuleta manufaa na kuwawezesha wafanyabiashara kuwanya biashara kukuza uchumi wa nchi na mtu mmoja moja.

Amesema katika mazungumzo hayo pia wamezungumzia kuhusu mazao ya kimkakati hasa katika kuchakata na sio kuuza malighafi, na hatimaye mazao hayo yachakatwe hapa nchini na kuuza bidhaa badala ya kuuza malighafi, na sekta ya matunda ambayo yanapatikana kwa wingi hapa nchini.

Nae Waziri wa Uwekezaji Mhe. Geoffrey Mwambe amesema katika mazungumzo hayo pia wamezungumza kuhusu uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwamo ya afya hapa nchini, na wameonekana kuridhika na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika uwekezaji.

Amesema wawekezaji kutoka Marekani wameonyesha wapo tayari kuja kuwekeza hapa nchini ambapo tayari kuna kampuni imeonyesha nia ya kuja kuwekeza katika sekta ya mawasiliano kwa kuwekeza katika kampuni ya simu, na kampuni ya utalii kutoka Arusha imeonyesha nia ya kutaka kuongeza zaidi uwekezaji.

Ameongeza kuwa “Tumeongelea uchakataji wa mazao na ukiangalia Marekani ananunua korosho nchi flani, na ukiangalia sisi tunauza korosho ghafi na hizo nchi zinachakata na kuuza marekani, na sisi sasa tunaweza kuzichakata hapa nchini na kuuza Marekani” amesema Waziri Mwambe.

Amesema pia yapo mazao mengine ya kumkakati kama Kahawa na Pamba ambayo yatachakatwa na kuuzwa nje ya nchi hatimaye kama nchi kupata mapato kupitia kodi na kukuza ajira kwa wananchi ambao watapata ajira katika viwanda hivyo vitakavyoanzishwa.

Amesema katika mazungumzo hayo wamekubaliana kufanya majadiliano mara kwa mara ili kuuisha makubaliano yao ambapo watakuwa wakifanya tathmini kuona makubaliano hayo yanavyofanya kazi katika kuimarisha ushirikiano uliopo kwa miaka sitini sasa baina ya haya mataifa mawili.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...