Search This Blog

Sunday, April 25, 2021

TAKUKURU Manyara yamshikilia mwendesha mashtaka kwa Rushwa

MWENDESHA mashtaka wa Mkoa wa Manyara, Mutalemwa Kishenyi anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Manyara, kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni tano.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara, Holle Joseph Makungu ameyasema hayo Mjini Babati wakati akizungumza Aprili 25, mwaka huu.

Makungu amesema kwamba Mwendesha mashtaka huyo wa Mkoa wa Manyara, wakili  Kishenyi amekamatwa  Aprili 23 mjini Babati usiku akiwa anapokea  kiasi cha shilingi milioni tano kwa watuhumiwa wa makosa ya jinai.

Amesema watuhumiwa hao walikamatwa katika upekuzi uliofanywa na mamlaka za dola  ambapo walikamatwa  na risasi 370 na stika bandia zenye thamani ya shilingi bilioni sita.

Mkuu huyo wa TAKUKURU amesema kuwa Mwendesha mashtaka huyo alikamatwa wakati akipokea rushwa ili kuwasaidia watuhumiwa hao.

“Uchunguzi zaidi wa tuhuma hizi unaendelea na ukikamilika mtuhumiwa huyu atafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma husika,” amesema Makungu.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...