Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesitisha shughuli za usafiri wa baharini zikiwemo safari za meli na vyombo vingine vya usafiri baharini kuanzia leo Jumamosi Aprili 24, 2021 saa 3 asubuhi.
Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Aprili 24, 2021 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Dk Khalid Salum Mohamed inaeleza kuwa Serikali imesitisha shughuli hizo kuchukua tahadhari ya kimbunga Jobo kinachotarajiwa kupiga mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Lindi, Mtwara na kisiwani Zanzibar pamoja na Mafia kesho Jumapili Aprili 25, 2021.
Inaeleza kuwa katazo hilo litadumu hadi hadi pale taarifa nyingine zitakapotolewa na mamlaka husika.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) kimbunga jopo kitajwa kuwa kitakuwa na mvua kubwa katika baadhi ya maeneo na upepo mkali unaovuma kwa kasi ya kilometa 60 kwa saa na kitasababisha mawimbi yenye urefu hadi wa mita 2 na nusu.

No comments:
Post a Comment