Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira imetenga Sh 300milioni katika mwaka 2021/22 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza kazi mbalimbali ikiwemo kukusanya sampuli za mafuta ya kwenye transfoma Zanzibar na kusafirisha Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo ameyasema hayo leo Aprili 27 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Jafo amesema kazi nyingine zitakazofanyika ni kukamilisha rasimu ya Kanuni za Usimamizi wa kemikali zinazodumu kwenye mazingira kwa muda mrefu (POPs) na ukusanya sampuli za hewa na kusafirisha nje ya nchi kwa uchunguzi wa kimaabara.
Nyingine ni kukusanya sampuli za maji na kufanya uchunguzi wa kimaabara nchini, kuwezesha uanzishwaji wa kanzidata ya kemikali zitokanazo na uchomaji taka na Kufanya kikao cha wadau cha kuainisha fursa za urejelezaji wa taka ngumu.
No comments:
Post a Comment