Search This Blog

Thursday, April 8, 2021

Rais Nguesso kuongoza tena Jamhuri ya Kongo



Rais Denis Sassou Nguesso ameidhinishwa kuingia tena uongozini katika nchi ya Jamhuri ya Kongo.

Katika taarifa iliyoandikwa, Mkuu wa Mahakama ya Katiba Auguste Iloki aliidhinisha ushindi wa Nguesso, ambaye alichaguliwa kwa kupata asilimia 88 ya kura kwenye uchaguzi wa urais uliofanyika Machi 21.

Iloki alisema kuwa pingamizi za wapinzani kwamba Nguesso hawezi kuchukua kiti cha urais zilichunguzwa na kufutiliwa mbali kwa kukosa kuwa na msingi.

Ushiriki katika uchaguzi huo ambao Nguesso alichaguliwa tena kuwa rais kwa kipindi cha miaka 5, ulikuwa ni asilimia 67.55.

Wajumbe wa ufuatiliaji wa uchaguzi wa Jumuiya ya Afrika walitangaza kuwa kulikuwa na usumbufu katika mchakato wa uchaguzi, ambapo viunganishi vya mtandao vilikatwa kote nchini.

Nguesso mwenye umri wa miaka 77 na ambaye ni mmoja wa marais waliodumu kwa muda mrefu zaidi barani Afrika, alitangaza kugombea tena mnamo Januari 24.

Mara ya mwisho, Nguesso aliingia tena kuongoza nchi hiyo yenye watu milioni 5, baada ya kushinda asilimia 60 ya kura katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2016 na kutawala muhula wa miaka 5.

Nguesso, ambaye amekuwa akitawala nchi hiyo tangu mwaka 1997, pia aliwahi kuingia madarakani kama rais katika kipindi cha kati ya mwaka 1979-1992.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...