Search This Blog

Sunday, April 11, 2021

Namungo yapoteza mbele ya Nkana kombe la shirikisho


 NAMUNGO FC Wawakilishi  wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika,walipoteza kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Uwanja wa Levy Mwanawasa, Zambia, ukiwa ni mchezo wa nne wa michuano hiyo hatua ya makundi ambapo timu hizo zipo Kundi D.

Dakika 90 zilikamilika kwa ubao kusoma Nkana FC 1-0 Namungo na kufanya ipoteza jumla ya mechi zote nne ambazo imecheza mpaka sasa na ipo nafasi ya nne bila pointi.

Katika mchezo uliopita baina ya timu hizo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, Namungo ilikubali kichapo cha bao 1-0.

Akizungumza na Saleh Jembe, Morocco amesema:"Ni uzoefu ambao unatupatia shida na kutufanya tusipate matokeo mazuri.

"Mapungufu ambayo tunayaona tutayafanyia kazi ili kupata matokeo kwenye mechi zetu zijazo," .

Bao la ushindi kwa Nkana FC lilipachikwa na Fredy Tshemega dakika ya 71.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...