Search This Blog

Sunday, April 11, 2021

Mwanamfalme Philip atazikwa wiki ijayo

 


Mazishi ya mume wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza, Mwanamfalme Philip, yatafanyika wiki ijayo. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kasri la Buckingham, mazishi hayo yataendeshwa kwa taratibu tofauti kutokana na vizuizi vya kupambana na janga la virusi vya corona. 


Shughuli ya mazishi itarushwa moja kwa moja kupitia televisheni, Aprili 17, saa nane mchana, katika kanisa la Mtakatifu George, magharibi mwa London. Mjukuu wake, Harry, ambaye kwa siku za karibuni, yeye na mkewe Meghan wamekuwa na mzozo na familia ya kifalme, atahudhuria mazishi hayo, ambayo yatawashirikisha watu 30 tu wa karibu. Bendera zitapepea nusu mlingoti kwenye majengo ya serikali hadi baada ya mazishi. 


Mwanamfalme Phillip, aliyekuwa mume wa Malkia Elizabeth kwa kipindi cha miaka 73, alikufa juzi Ijumaa akiwa na umri wa miaka 99.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...