Search This Blog

Sunday, April 25, 2021

Moto uliozuka katika hospitali ya corona Iraq: Watu 82 wafariki baada ya 'tangi la Oksijeni kulipuka'


Takriban watu 82 wamefariki katika moto uliozuka katika hospitali ya kutibu wagonjwa wa Covid 19 katika mji mkuu wa Iraq Baghdad.

Zaidi ya watu 100 walijeruhiwa katika moto huo uliozuka katika hospitali ya Ibn Khatib siku ya Jumamosi usiku.

Ripoti zinasema kwamba ajali ilisababisha tangi la oksijeni kulipuka na kusababisha moto huo.

Kanda za video zinaonesha wazima moto wakijaribu kuuzima moto huo huku watu wakitoroka jumba hilo.

Waziri mkuu wa Iraq Mustafa al-Kadhimi alitoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi wa haraka kuhusu chanzo cha kile alichokitaja kuwa ajali mbaya.

Mkuu wa ulinzi wa umma Jenerali Kadhim Bohan, alisema kwamba moto huo ulianzia katika chumba cha wagonjwa mahututi katika ghorofa iliotengwa kuwasaidia watu kupumua.

Takriban wagonjwa 30 walikuwa katika chumba hicho cha wagonjwa mahututi kilichotengewa watu waliokuwa hatarini na corona mjini Baghdad, chanzo kimoja cha hospitali kiliambia chombo cha habari cha AFP.

Wagonjwa wote wamehamishwa katika hospitali iliopo karibu.

Moto huo ulidhibitiwa mapema siku ya Jumapili , alisema mkuu wa ulinzi wa umma nchini humo.

Gavana wa mji wa Baghdad Mojammed Jaber aliunga mkono wito wa waziri mkuu kuhusu kufanyika kwa uchunguzi wa haraka ili kubaini iwapo kuna mtu yeyote anayepaswa kuchukuliwa hatua.

Katika taarifa , tume ya haki za kibinadamu inayomilikiwa na serikali imesema kuwa tukio hilo ni uhalifu dhidi ya wagonjwa waliochoshwa na ugonjwa wa corona.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...