Search This Blog

Thursday, April 8, 2021

Marais sita wapanga mkutano wa dharura juu ya mgogoro wa Msumbiji


Viongozi sita wa Afrika watakutana katika mji mkuu wa Msumbiji , Maputo,ambapo kutakuwa na mkutano wa dharura unaoangazia mashambulizo yanayotokea kusini mwa Afrika, tovuti ya serikali ya Zimbabwe imeripoti.

Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) imeitisha mkutano huo na Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi. Ukiondoa Msumbiji ambaye ndio mwenyeji, mataifa mengine yatakayokuepo katika mkutano huo ni Afrika Kusini, Botswana, Zimbabwe, Malawi na Tanzania.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnagngawa tayari ameondoka katika kikao hicho.

Awali rais wa Msumbiji Filipe Nyusi alisema ataitisha mkutano wa baraza la ulinzi na usalama lakini hakuweka wazi ni lini mkutano huo utafanyika.

Wanamgambo wa kiislamu walivamia mji wa Palma uliopo kaskazini mwa jimbo la Cabo Delgado Machi 24, na kuuwa watu kadhaa na mamia kulazimika kukimbia makazi yao huku wengine wakikimbilia Tanzania.

Kundi la wanamgambo wa kiislamu (IS) walidai kuhusika na shambulio hilo.

Kundi hilo la wanamgambo wa kiislamu limlenga eneo hilo tangu Oktoba mwaka 2017, na hivi karibuni shambulio lao lililazimisha kampuni kubwa ya nishati ya Ufaransa kusitisha mipango yake ya uzalishaji wa gesi asilia katika eneo la Afungi Peninsula.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...