Raia wa Chad wamepiga kura kumchagua rais huku Idriss Deby Itno akitarajiwa kushinda muhula wa sita baada ya miongo mitatau madarakani.
Deby mwenye umri wa miaka 68 ndiye anayepigiwa upatu kuebuka mshindi katika uchaguzi huo ulio na wagombea sita ambapo hakuna anayempa ushindani mkubwa.
Baadhi ya wanasiasa wa upinzani walitoa wito wa uchaguzi huo kususiwa jambo linalozua maswali kuhusiana na idadi ya watu waliojitokeza kushiriki.
Lakini mara baada ya kupiga kura yake, Deby, alitoa wito kwa Wachad kujitokeza kwa wingi kote nchini humo na kupiga kura.
Vituo vingi vilivyotembelea na shirika la habari la AFP vimeshuhudia upigaji kura kuanza kuchelewa kutokana na ukosefu wa vifaa na polisi walikuwa wanapiga doria katika mji mkuu N'Djamena.

No comments:
Post a Comment